Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka
2012, Walter Chilambo ana ushauri kwa Nay wa Mitego. Afanye uchunguzi na
utafiti wa kina kabla ya kuongea mambo kwenye nyimbo zake.
Bongo5 ilikaa na staa huyo wiki
iliyopita kuzungumzia wimbo wa Nay wa Mitego, Salam Zao ambapo alisema
Walter amepigika licha ya kuwa mshindi wa milioni 50 mwaka jana.
“Kwangu kidogo alikuwa wrong kwasababu
mimi sipo hivyo yeye anavyozungumza, inabidi angefanya uchunguzi kwanza
kwamba sina hata baiskeli au naishi vibaya au siwezi kula, siko poa,
angefanya uchunguzi kwanza halafu ndio angeongea,” alisema Walter.
“Lakini mimi simlaumu, kaongea ambacho yeye anakifeel.”
Katika hatua nyingine, Walter amesema yupo mbioni kufanya video ya wimbo wake wa sasa, Doro.
Source:Bongo5
No comments:
Post a Comment