05 February 2016

UMESKIA MADUDU MENGINE YA TFF....? NDO HAYA HAPA ...

Shirikisho la soka nchini TFF leo imefanya maajabu mengine baada ya kubadili ratiba ya Ligi Kuu ya mechi ya JKT Ruvu na Mbeya City kwa kuianzisha mapema ili kupisha mechi ya kirafiki kwenye dimba la Karume jijini Dar es salaam.

Kwa kawaida ratiba ya mchezo huo ilikuwa inaonesha kwamba JKT Ruvu na Mbeya City ni saa 10 jioni lakini TFF ikaurudisha nyuma mchezo huo na kuufanya uanze saa 9 alasiri kwa lengo la kupisha mchezo wa kirafiki usiotambulika na TFF kati ya Clouds Media na Majaji.
Mabadiliko hayo yamezua malalamiko mengi katika mitandao ya kijamii huku wengine wakidai kwamba viongozi wa Shirikisho hilo wameshindwa kuongoza soka la Tanzania.
Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita TFF ilifanya kosa kwa kuiruhusu Azam FC kuacha mechi zake za Ligi kuu na kwenda nchini Zambia kucheza mechi za kirafiki, jambo ambalo Rais Jamal Malinzi aliomba radhi.
Katika mchezo huo wa leo kati ya JKT Ruvu na Mbeya City, Mbeya imeshinda mabao 2-1

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname