Wimbo wa Happy wa Pharrell Williams ulikuwa moja ya nyimbo
ninazosikiliza kila ninapo amka asubuhi, kwanini sababu ni siku mpya na
nilitaka kuanza na furaha kama jina la nyimbo. Je, wewe unafanya nini
cha kwanza unapoamka asubuhi.? Kuna vitu vidogo sana unaweza ukawa
unafanya kila siku na ukajisikia mwenye furaha na ukaanza siku yako
vizuri
Usizime Alarm (kengere).
Kuna wakati unahitaji kitu cha kukufanya uamke muda unaopanga wewe
asubuhi. Kengere ya simu au saa ya mezani, inapoita wengi wetu sababu ya
usingizi mwingi tunaizima na kuendelea na usingizi, kwa dakika chache,
ila ni vizuri kama ulipanga kuamka muda huo basi na uamke . panga
ratiba yako na uizoe.
Tafuta Ujumbe wa kukupa moyo.
Kuna wakati tunahitaji mtu wa kutuambia tunaweza,weka chumbani kwako
ujumbe mzuri wa kukupa moyo kama “You’re the Best” au unaweza ukaingia
Google na kutafuta “inspiration quotes” hizi ni nikuu za watu
mbalimbali, ambazo unaweza kusoma kila unapo amka uanze na siku
mpya.kila siku mpya ni zawadi na unatakiwa uwe na mwanzo mpya sababu
siku hazifanani.
Kaa mbali na tekinologia kwa muda wa saa moja.
Hapa naongelea Tv,radio au simu. Simu ni kitu cha kwanza mtu akiamka
anashika asome ujumbe, aingie kwenye mitandao ya kijamii
Facebook,Twitter and Instagram si kitu kibaya kwenda na wakati nakujua
nini kinaendela duniani, lakini chukua muda wa saa moja fanya mambo
mengine na ufanye kama unahisahau simu kwa muda.
Fanya mazoezi.
Kuna watu wanasingizia muda inapokuja swala la mazoezi, please, dakika
20 tu zinatosha kufanya mazoezi ukiwa nyumbani, sijui watu wengine
wanatumiaje mitandao ya kijamii, kama instagram na Youtube kuna video
zinaonyesha aina ya mazoezi unaweza ukafanya ukiwa nyumbani hii ni
rahisi kwa mtu yoyote kufanya mazoezi akiwa nyumbani, mazoezi yanasaidia
kupunguza stress na kusaidia mzunguko wa damu.
Pata kifungua kinywa.
Kwa kawaida tunakula mara 3 kwa siku ila kwa mara zote 3, kifungua
kinywa ndo mlo wa muhimu kuliko yote, pata chai au kikombe cha kahawa
kila siku asubuhi hautojuta,
Pangilia Ratiba yako ya siku.
Hili ni tatizo kwa wengi , mtu anaanza siku kama zali tu hajui anaanza
na nini au wapi anaanza siku yake na kama ni mtu anafanya kazi ofisini
hata hajui anaanza na kazi gani akifika ofisini,lazima uwe na ratiba
ujue unaanza na nini na unamaliza na nini. Hii itakufanya ufanye mambo
yako kimpangilio zaidi.
Wajibika.
Wajibika katika majukumu yako,ukiwa na kazi ni rahisi kuona siku inaisha
kirahisi na haraka uwe mama wa nyumbani, unafanyakazi ofisini ama we ni
kaka muuza genge zote kazi cha msingi ni kujari muda na kupenda kazi
yako ukiwa mtu wa kuwajibika hautokuwa na muda wa kufanya vitu visivyo
na maana au kama mwanamke kujiingiza katika matatizo au vikundi vya
kimbea.
No comments:
Post a Comment