20 April 2014

TAFSIRI YA TATTOO ZA DIAMOND, UWOYA, WEMA NA MASTAA WENGINE WA BONGO


unnamed3
Kama tungekua nchi za wenzetu tukaanza kuandika kuhusu tattoo na wasanii basi tusingemaliza leo, maana karibia kila msanii ana tattoo na sio moja tu bali zaidi ya moja. Lil Wayne ana zaidi ya tattoo 300 , Rihanna ana tattoo 19 ,Miley Cyrus ana tattoo 19 na Bruno Mars akiwa na Tattoo 5 . Tattoo imekua ji mfumo ambao wasanii wengi sana duniani wamekua wakiutumia kuandika miili yao kwa maana fulani au basi tu urembo, kuna wasanii kama Birdman “Baby” Cash Money Records CEO ambae yeye na mwanae wa kufikia Lil Wayne wana tattoo mpaka usoni kuchora matone ya MACHOZI kwa kila mtu ambae ni muhimu kwao aliewatoka (kufariki) na hii ni kumaanisha kuwa bado wanawalilia. Kwa mujibu wa wataalam wanasema Tattoo ni “Addiction” ukianza na moja tu, utajisikia kuchora nyingine na nyingine na utakuta zinaongezeka mwilini na hii ni sababu ya kupenda zinavyoonekana au starehe ya maumivu wakati inachorwa.


Lakini vipi kwa upande wa bongo? Tattoo na usanii au umaarufu vimeanza kuendana hapa bongo baada ya sanaa kuanza kutambulika na sana sana ya wasanii wa BongoFlava, zamani tattoo walikua wanachora Mabaharia wanaofanya kazi kwenye Meli kubwa na wao walikua wanaiga desturi za hao wanaowaajili kwenye Meli hizo, kwa hiyo kwa hapa nchini kuanzia miaka ya 80 tattoo maarufu sana zilikua “NANGA” ya Meli, Nyoka ajulikanae kama “COBRA”, “bleeding Heart”, “Eagle” na hizi zote zilikua ni tattoo zilizoletwa na Mabahari watanzania wafanyao kazi kwenye Meli za Kigiriki na nyinginezo za Bara la Ulaya.
Hii ni list ya wasanii wa bongo wenye tattoos.
unnamed
Diamond Platnumz
Diamond PLATNUMZ ana tattoo kubwa kwenye mkono wake wa kulia maeneo ya begani na nyingine kwenye mkono wake wa kushoto yenye maandishi ya kichina ambayo maana yake ni “I Love U Mama”, sijui ni kwanini ameamua kuandika kwa Lugha ya kichina ila kwa maoni yangu ingependeza zaidi kama angetia lugha anayoitumia yeye ya nchini kwake kama “Nakupenda Mama” ingependeza zaidi.
unnamedk
Wema Sepetu
Wema SEPETU ni moja kati ya wasanii wa bongo wenye tattoo nyingi , ana tattoo kwenye shingo yake , pia ana tattoo yenye maandishi ya kichina mgongoni yenye maana ya “potential” kwa lugha ya kiingireza. pia ana tatoo mkononi na kwenye bega. na zaidi ya hapo hana tattoo nyingine sehemu ambayo inaonekana wazi labda kwingine ambako hatuwezi kuona au kuonyesha kwenye PUBLIC maana katika mwili wa binadamu kuna sehemu “Potential” nyingi sana ambazo tattoo inaweza kukaa vizuriiii kabisa na kuonyesha MVUTO wa hali ya juu.
unnamed3
Ney wa Mitego
NEY Wa MITEGO ni mmoja kati ya wasanii wabishi wanaofanya muziki mgumu maarufu kama Hip Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama msanii anayetafsirika kimuonekano, Ney wa mitego ameanza kuchora tattoo tokea mwaka 2002 alipokua kidato cha pili katika shule ya sekondari ya mbezi beach. Katika mkono wake wa kulia kuna tattoo yenye nanga ya “HIP HOP” ikiwa na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani na ndoto za kufanikiwa kupitia muziki huo wa ‘Hip Hop’, ‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa kushoto ni nyoka mwenye mabawa (Dragon) , Dragon ni kiumbe ambacho ni adimu kuonekana duniani na kinachoabudiwa sana barani Asia sana sana China na Korea.
.
unnamed4
Elizabeth Michael “Lulu”
ELIzABETH “Lulu” MICHAEL naye hayupo nyuma katika kuchora tattoo. Lulu ni msanii ambaye anakua ndani ya sanaa na ana fursa kubwa sana kujifunza mambo mengi taratibu kutokana na Umri wake na ukuaji wake ndani ya sanaa, Lulu ni msichana ambae tunamtegemea sana kufikisha tasnia hii ya Filamu mbali sababu kwake yeye ni kama yupo Darasani maishani kusoma maisha na tasnia pia. Ni matarajio makubwa sana aweze kujifunza vyema na kuweza kuifikisha Tanzania katika nyanja za juu za Filamu kama wasanii Lupita Nyongo wa Nchini Kenya. kwa upande wa Lulu ni kidogo na ni tofauti na wengine kwani yeye ameamua kuweka ujumbe wa maneno chini kidogo ya shingo lake karibia na bega unaosema “Only God can Judge Me” hii inamaanisha ni “Mungu Pekee ndio atakae nihukumu”
.
unnamed5
Jux
Jux VUITTON ana tattoo mbili, Ya kwanza ipo kifuani na watu wengi wamekuwa wanasema tattoo hii inafanana na ile ya “Trey Songz” msanii wa mindoko ya RNB nchini Marekani ambae nae aliwahi kushukiwa kuwa style yake ya uiambaji anamuiga msanii mkongwe wa miondoko hiyo R KELLY. Tattoo hiyo ya JUX lakini ukweli ni kuwa sehemu ya mwili  aliyoichora ni kama ya msanii Trey Songz lakini fonts na ujumbe ni tofauti kwani tattoo ya msanii huyo ameandika ameandika kwa ajili ya mama yake , mdogo wake wa kiume na bibi yake huku kwa upande wa JUX ukiwa na ujumbe mzito pia lakini hatujajua bado unamhusu nani na part ya tattoo hiyo inasema “ALWAYS MISSING YOU” na “HOPE TO SEE YOU”. Jux ana tattoo nyingine mkononi maeneo ya bega ikiwa na “Virgo Angel” kwa kibongo tunaweza ambayo kwa lugha ya kiswahili inajulikana kama mashuke .
unnamed55
Irene Uwoya
Irene UWOYA nae ni kati ya wasanii wakubwa wakwanza kabisa kunyesha tatoo zake katika mwili wake, UWOYA ana tattoo juu kidogo ya matiti yake yenye alama ya nyayo za paka au chui ambapo tattoo hii ilikua maarufu sana miaka ya 90 ambayo tattoo hiyo ilivhorwa na mwanadada msanii wa miodoko ya Hip Hop nchini Marekani “EVE”. Tattoo hii ilikua maarufu sana na wanadada wengi sana duniani waliweza kuchora tattoo hii sababu ndio ilikua HOT kipindi hicho kutokana na msanii huyo. Pia UWOYA ana tattoo mgongoni  iliyoandikwa krrish ikiwa na alama za nyayo ya mtoto mdogo ambayo ni maalumu kwa ajili ya mtoto wake Krrish Ndikumana. Kuna tattoo nyingine zinaonekana kiunoni na miguuni pia ila sehemu nyingine zinahitaji kazi kubwa sana kuweza kuziona vizuri na kuweza kupata maelezo kamili au hata picha zake ili kuweza kushare na wasomaji

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname