07 February 2016

;HIVI NDIVYO WAHINDI WANAVYOWANYANYASA NA KUWADHALILISHA WAAFRIKA NCHINI INDIA

 
Waafrika wanaishi kwa shida sana nchini India.Unaweza kupigwa na kudhalilishwa mbele ya polisi na bado usisaidiwe kwa lolote.
Unaweza kuwa unatembea barabarani Muhindi akaamua tu kukutemea mate.Nakumbuka siku moja nilipita nje ya gate la Muhindi. Akaamua tuu kufunguliwa Mbwa wake wanikimbize....Nilikimbia huku Mbwa wakiwa wananifukuza. Nikaanguka chini na kuchanika mguuni.

Mimi na rafiki zangu tuliishi kwa kunyanyasika sana India. Tulikuwa tunashikwa makalio na madreva Bajaj NK.Hayo mambo machache yalinifanya niichukie sana India.

Watu wengi huwa wanakutana na civilized Indians. Inakuwa si rahisi kujua ubaya wao. Lakini si watu....Nawaambia Indians ni watu wa ajabu sana jinsia unavyowaona sivyo walivyo.

Siku moja nilishuhudia Mwafrika kutoka Ivory Coast akitumbukizwa kwenye shimo la maji machafu yenye kinyesi.Sijawahi kumshauri Mtanzania yeyote ampeleke mwanae India kwa masomo.
SOURCE-JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname