17 January 2016

Nuh Mziwanda: Nilishaficha Mambo Mengi Sana Mabaya ya Shilole kwa Maslahi ya Penzi Letu

Nuh Mziwanda amedai kuwa aliyofanyiwa na Shilole ni mengi na mazito ambayo ilibidi ayafiche kwa maslahi ya penzi lao na heshima kwake.
shishi na Nuh m
Akiongea kwenye kipindi cha D’Weekend Chat Show cha Clouds TV Ijumaa hii mbele ya Shilole aliyekuwa amejikunyata pembeni kwa kukasirishwa na uwepo wa ex wake studioni hapo bila kutaarifiwa mwanzoni, Nuh alisema Shilole hakuwa mwanamke wa kutawaliwa.
“Yeye anajua mambo gani alikuwa anafanya kwangu mambo ambayo yalikuwa hayastahili anifanyie. Alikuwa anafanya kwa kunichukulia poa kwamba nitafanya nini lakini at end of the day kila kitu kina mwanzo na mwisho,” alisema.
Nuh alisema ni ngumu tena kurudisha imani kwa mpenzi wako huyo licha ya kukiri kuwa bado hajaweza kuwa tayari kuwa na mwanamke mwingine kwa sasa.
Chanzo: Bongo5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname