17 January 2016

BREAKNG NEWZZ......Watu 3 wamefariki na 35 kujeruhiwa katika jali ya basi eneo la Kiyegeya mkoani Morogoro.


 
Watu watatu wamefaiki dunia na wengine 35 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyohusisha basi la Kiruto Express likitokea Kondoa kwenda Dar es Salaam wakati dereva wa basi la Site Boy kutaka kulipita gari lingine bila tahadhari katika eneo la Kiegeya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Wakizungumza na ITV mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo kondakta wa basi lililopata ajali wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa sita mchana wakati basi hilo likitokea wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo wameeleza ajali hiyo ilivyotokea.
ITV ilifika katika hospitali ya misheni ya Berega walikolazwa majeruhi wa ajili hiyo ambapo mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta Bahati Chiponda amekiri kupokea mili miwili na majeruhi 35 na kwamba majeruhi mmoja amefariki wakati akipatiwa matibabu na kupelekea idadi ya waliopoteza maisha kufikia watatu huku majeruhi wengine bado hali zao zikiwa ni mbaya

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname