Nimegundua Mabinti Wanashindwa Kutofautisha Mume na Boyfriend-JB
Nakaribia 50 sasa na huku mtaani kwetu nimepewa heshima
ya mzee wa mtaa… na kila j2 jioni huwa nasuluhisha kesi za wana
ndoa…katika kesi nyingi nimegundua mabinti wanashindwa kutofautisha mume
na mwanaume wa starehe (boyfriend) na ndio maana una weza ukaenda
harusini watu wakabeza aiii kampendea nn??? Anamefata hela tuu…sababu
kuna vitu mnaviangalia ambavyo si sifa za mume…ni ziada tu ambayo kama
itakuwepo una bahati…mume anatakiwa awe na sifa nyingi lakini kuu ni
kuwa macho…masikio…mikono na moyo wake utakuwa kwa mke wake bila kujali
wanawake wangapi wazuri wanamwinda…na yuko tayarikuihudumia na kuingalia
familia yake…sio lazima awe giant na hb kama jb…wanawake wengi
wameishia kuzalishwa na kuachwa na kutengeneza watoto wengi wasio na
malezi ya baba na mama…na hawa walioachwa ss wana chuki kubwa na
wanaume….pia kizazi hiki cha kuanzia miaka 30 kwenda chini kina wanawake
wengi wajeuri wenye kujiamini kupita kiasi…nionavyo huko mbele ndoa
zitakuwa chache…wacha nile pilau yangu nijiandae saa 10…kuna wengine
wanakuja washatibuana karibia wiki3 sasa
By Jb on Instagram
No comments:
Post a Comment