kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata
akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari
kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu
Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata
akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji
wa mapato wa kila mwezi.Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kiasi
hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi
ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba
ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa
mwezi.
Takwimu
hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi
nchini.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.
Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.
Kidata
amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya
kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato
na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika
vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
Katika
hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya
shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara
walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.
Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Dar es Salaam
6.1.2016
No comments:
Post a Comment