09 January 2016

BREAKING NEWS: MAYANJA KOCHA MSAIDIZI SIMBA

Na Sheila Ally
KOCHA Jackson Mayanja aliyekuwa akiifundisha Coastal Union ya jijini Tanga leo ametua Simba kuwa msaidizi wa Dylan Kerr ambaye hakupata msaidizi tangu Seleman Matola ajiuzulu.

Mayanja ametua leo mchana na kuungana na kikosi cha Simba kilichopo visiwani Zanzibar ambako kinashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na kesho watacheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.


Habari za uhakika ambazo BOIPLUS imezipata kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa kocha huyo amemalizana na vigogo hao na ataanza kazi mara moja japokuwa Kerr ametaka kuangalia kwanza CV zake.

''Ametua mchana wa saa 8 na ameunganisha Zanzibar ni kocha mzuri na tunaamini kwa ushirikiano wake na Kerr timu yetu itakuwa imara zaidi, kila kitu kuhusu Mayanja kipo vizuri,'' alisema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo amesema kesho huenda kocha huyo atakuwepo kwenye Benchi la Ufundi wakati wa mechi yao ya nusu fainali.

Mayanja amewahi kuifundisha Kagera Sugar kwa mafanikio makubwa na tangu aondoke timu hiyo imekuwa ikisuasua kwenye ligi hata Coastal Union haijafanya vizuri ingawa sababu kubwa ni za kiutawala.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname