SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kuicheze timu ya taifa,
Taifa Stars dhidi ya Uganda Jumamosi.
CAF imeiambia TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwamba Ngassa haruhusiwi
tena kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kwa
sababu siyo tena mchezaji wa Ligi ya nchini mwake.
Ngassa aliyesaini Mkataba wa miaka minne na Free State Stars ya Afrika
Kusini Mei mwaka huu akitokea Yanga SC ya Tanzania kwa sababu hiyo
ameondolewa kikosini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo
wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN
2016.
Mrisho Ngassa amezuiwa na CAF kucheza dhidi ya Uganda Jumamosi
Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7
ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda
utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia
majira ya saa 2 usiku.
Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu
kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)
zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili
baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea
na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa
Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao
hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji
wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN
wikiendi hii.
Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga,
Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias
Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey
Morris na Nadir Haroub.
Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank
Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.
Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao
ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda),
Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na
kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya
No comments:
Post a Comment