19 December 2015
Wanafunzi 500,000 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza
Hata hivyo, wanafunzi 12,847 kati ya hao waliofaulu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara, wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 503,914 kati ya 518,034 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa kupata alama A, B na C, wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za sekondari za Serikali katika awamu ya kwanza. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.3 ya wanafunzi waliofaulu na wenye sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Hata hivyo, wanafunzi 12,847 kati ya hao waliofaulu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara, wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Akitangaza matokeo hayo jana Dar es Salaam, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jaffo alisema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2016 ni 503,914 kati yao, wasichana ni 255,843 sawa na asilimia 99.2 na wavulana 248,071 sawa na asilimia 97.7.
Alisema takwimu hizo zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza imeongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2015.
“Wanafunzi 610 sawa na asilimia 61.2 ya wanafunzi 997 wenye ulemavu waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wamefaulu na wote wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari na ufaulu wao ni sawa na ongezeko la asilimia 0.6 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2014,” alisema Jaffo.
“Naagiza mikoa na halmashauri zenye wanafunzi hawa 12,847 ambao wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza kuhakikisha kuwa wanakamilisha vyumba vya madarasa kabla ya Machi mwakani ili kuwezesha wanafunzi hawa kujiunga na kidato cha kwanza,” alisema Jaffo.
Sh18.7 bilioni kila mwezi
Katika hatua nyingine; Jaffo alisema Serikali imetenga Sh18.77 bilioni kwa kila mwezi kuanzia mwezi huu hadi Juni 2016 kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shule za Serikali kuanzia ngazi ya msingi hadi kidato cha nne ikiwa ni pamoja na chakula cha wanafunzi kwa shule za bweni na ada
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment