Diamond Platnumz – Tanzania.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo ya MTV Africa Music Awards 2015: Best Live Act pamoja na MTV EMA 2015: Best African Act, Diamond Platnumz kwa mwaka huu ametajwa kama mmoja wa wasanii wa kubwa wa Africa kwa
mwaka 2015 akiwa na ushawishi mkubwa ndani na nje ya Africa, akiwa pia
na mashabiki wakubwa na wanaomuongelea zaidi kwenye mitandao ya kijamii
kitendo kinachomfanya Diamond kuwa msanii kijana mwenye ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2015.
Yemi Alade – Nigeria
Baada ya hit song yake ya ‘Johnny’ kuweka headlines sehemu mbalimbali Africa staa wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade alijipatia umaarufu mkubwa sana kupitia video hiyo ambayo ushawishi wake umegusa watazamaji zaidi ya milion 30 kweye mtandao waYouTUBE. Ukiachia hayo style yake ya muziki pamoja na mavazi yake imetokea kuvutia wasichana wengi wanaofuatilia muziki wake.
Koffi Olomide – DRC Congo.
Mkongwe wa muziki kutoka Congo, Koffi Olomide amekuwa akijulikana kwenye industry ya muziki kuanzia miaka ya 1970 na bado umaarufu wake unagusa watu wengi wa rika zote duniani. Mwezi October mwaka huu 2015, Koffi aliachia album yake ya 13 na ya mwisho ikiwa na nyimbo 39. Licha ya kuachia Album yake ya mwisho Koffi anahesabika kama miongoni ya watu waliobadilisha sura ya muziki nchini Congo.
Trevor Noah – South Africa.
Mchekeshaji kutoka South Africa, Trevor Noah aliiteka dunia baada ya Marekanikumtangaza kuwa mtangazaji mpya atakayerithi kiti cha show ya comedy, The Daily Shownchini Marekani. Toka ujio wa Trevor Noah kwenye
kipindi hicho watazamaji wa show hiyo kutoka Marekani wametokea
kuvutiwa na mchekeshaji huyo ambaye material yake kubwa ya comedy
inaongelea sehemu kubwa ya maisha ya Kiafrika. Kwa mujibu wa ripoti
kadhaa zilizotolewa na mitandao tofauti Marekani, ujio wa Trevor Noah kwenye kipindi hicho kumeongeza watazamaji milion 1.5 kwenye show hiyo.
Lupita Nyong’o – Kenya.
Baada ya kushinda tuzo yake ya kwanza ya Oscars ya Best Supporting Role kwenye filamu yake ya kwanza kubwa, Two Years A Slave, staa wa movie Lupita Nyong’o kutokaKenya amezidi kuonyesha uwezo wake kwenye industry ya filamu Marekani kwa
kuzidi kupokea nafasi nyingi kubwa za kuigiza pamoja na kushinda tuzo
kadhaa kwenye majukwa mbalimbali Marekani. Licha ya hayo Lupita pia ni Balozi wa Wild Elephants na Mwanaharakati wa haki za Wanyama
No comments:
Post a Comment