Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba,
amewasimamisha kazi maofisa 10 wakiwamo wahasibu waandamizi na mafundi
kwa kusababisha upotevu wa mapato zaidi ya Sh.milioni 100.
Hasara
hiyo ilitokea katika mfumo wa mita kupitia minara ya simu za mkononi na
faini Sh. milioni 198.1 za wateja waliobainika kuiba umeme kwa
kuchakachua mita zao.
Hata
hivyo, shirika hilo limefanikiwa kuokoa fedha hizo zilizotokana na
umeme wenye thamani ya Sh. 100,248,386.42 uliotumika bila kulipiwa
pamoja na faini kutoka kwa wateja waliojihusisha na wizi wa umeme Sh.
198,105,928.68.
198,105,928.68.
Kadhalika,
shirika baada ya kufanya msako mkali limefanikiwa kukamata taasisi
binafsi na za serikali pamoja na watu binafsi wakijihusisha na kuhujumu
shirika hilo,ikiwemo Shule ya Sekondari ya Jangwani (Sh. 11,023,238.00),
Diwani wa Kata ya Sinza C, Joseph Marandu (Sh. 3,443,555.00), Royal
Oven Bakery Kawe, (Sh. 4,112,614.00), Havan Hotel, Mbezi Beach
(Sh.1,847,913.00) na Kampuni ya Simu ya Viettel Mtwara (Sh. 524,554.76).
Wengine
ni, Kampuni ya Saffa Petroleum ya Mkoani Pwani (Sh. 16,105,235.00),
Msanii wa Filamu Nchini, Wema Sepetu (Sh. 8,200,496.20) na Kampuni ya
Leadcom (Sh. 13,694,632.81).
“Zoezi
hili ni endelevu kwa nchi nzima na tutaendelea kuwakamata, kuwatangaza
na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale watakaobainikiwa kulihujumu
shirika hatutaogopa wadhifa wala umaarufu wa mtu ama taasisi” alisema
Mramba katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam.
Alisema
mapema Desemba 6, mwaka huu alitoa taarifa kwa wale wote wanaojihusisha
na wizi wa umeme ama wenye mita zenye matatizo, lakini walijisalimisha
ni watu 30 na kati ya watu 2,156 waliokaguliwa 138 walikutwa na dosari
mbalimbali katika mita zao na walilipishwa faini.
Akifafanua,
alisema fedha zinazotakiwa kulipwa ni Sh. milioni 198.1 na
zilizokwishalipwa ni Sh. milioni 44.9 wakati waliofikishwa kwenye vyombo
vya sheria ni watu 37 kwa makosa mbalimbali. Akizungumzia kuhusu hatua
atakazowachukulia watumishi 10 aliowasimamisha kazi, Mramba alisema
uchunguzi unaendelea na fedha wanazodaiwa kuzifanyia udanganyifu
zitalipwa na kampuni ya simu husika.
No comments:
Post a Comment