Maneno kuntu! Staa mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Isaac Sepetu
amefungua kinywa chake na kusema kuwa endapo Mgombea wa Urais wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa angeshinda kuwa
Rais wa Tanzania katika uchaguzi uliopita, bila hiyana yeye angehama
nchi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wema alisema kuwa anamshukuru Mungu kuwa
anasubiri kwa hamu kuapishwa kwa mshindi wa nafasi hiyo, Dk. John
Magufuli ambaye anamuamini ni mchapakazi asiyekuwa na urafiki na mtu
mzembe.
“Sifichi, kweli kabisa Lowassa angeshinda, bila ubishi ningehama nchi yangu niipendayo,” alisema Wema.
GPL

No comments:
Post a Comment