"Tangu
juzi kumekuwapo na tetesi kuwa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA, huenda umoja huu ukasambaratika kwa kile kinachoelezwa
kutokukubaliana kwa mgawanyo sawa wa majimbo kuelekea uchaguzi mkuu
Oktoba.
Imeripotiwa
pia leo vijana wa chama cha wananchi CUF na NCCR mageuzi, wanatarajia
kuandamana ili kushinikiza viongozi wa juu wa vyama vyao kuachana na
UKAWA kwa kile wanachokiita kupunjwa usawa wa uwakilishi katika majimbo
na CHADEMA.
Naibu
katibu mkuu wa CUF Tanzania bara, Julius Mtatiro amekuwa akitoa mtazamo
wake mara kwa mara kuhusu kadhia na migogoro hii ya UKAWA, akisisitiza
kutokukubaliana na kuvunjika kwao.
Timesfm.co.tz
imeunasa waraka aliouandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, ili
kufahamu kile ambacho anakifikiri kama kiongozi wa chama kinachounda
UKAWA.
“SHEREHE
ZA KUVUNJA UKAWA??? Ndugu zangu, Tangu jana nimeona MATAMKO ya watu
mbalimbali wakijinasibu kwamba ni bora UKAWA ivunjike, wengine wanasema
vyama vyao vinamezwa, wengine wanasema hawakubali hili na lile n.k.
bahati mbaya haya yasemwayo ni mambo ambayo viongozi wa juu wa UKAWA
ndiyo wanapaswa kuyashughulikia, si viongozi wa kawaida wa vyama au
wanachama.
Mimi
nataka tena kurudia kusema hapa, kwamba UKAWA ikivunjika kwa sababu
yoyote ile, ni KITENDO CHA VYAMA VYA UPINZANI KUWASALITI WANANCHI.
Hakuna lugha nyingine.
Na
wale wanaofurahia UKAWA ikitetereka na wanaoombea ivunjike waendelee
kuomba maombi hayo yasiyo na tija kwa taifa. UKAWA ikishavunjika vyama
vya upinzani havitabaki salama hata kidogo.
Athari
ambazo chama kimojakimoja kinazipata ndani ya UKAWA ni chache kuliko
chama kimojakimoja kikienda kivyake. UKAWA ilikuwa na malengo makubwa
sana, achilia mbali uchaguzi, kuna ajenda ya katiba.
Tuliondoka
kwenye bunge la katiba na kuacha milioni 30 kila mjumbe kwa sababu ya
kujenga mshikamano wa upinzani. Kuvunja UKAWA leo ni kusema pia
TUNAIKUBALI KATIBA inayopendekezwa. Tukivunja UKAWA leo
#Tutapigwa_kwenye_uchaguzi_mkuu_huu lakini zaidi ya yote
#Wananchi_Watatupiga_Mawe_Tutakapojipeleka_Kuwaambia_Waikatae_Katiba_Inayopendekezwa
kwani tutakuwa
#Hatuaminiki_Kwa_Mambo_Madogo_Na_Hatuwezi_Kuaminika_Kwa_Mambo_Makubwa.
Mimi
naamini katika USHIRIKIANO WA VYAMA VYA KIMABADILIKO ili kulikomboa
taifa, siamini kinyume chake hata kidogo. Kwa sababu viongozi waliahidi
leo ndipo wataamua mustakabali wa kila kitu, kila mpenda mabadiliko
anasubiri kwa hamu kujua viongozi wanaongoza tupite njia ipi. Mungu
awabariki nyote.” ameandika Mtatiro.
No comments:
Post a Comment