02 October 2014

BIFU LA FLORA, NISHA LAFIKA PABAYA!

WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama hawafahamiani.Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’. Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam. Wawili hao walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa meza yake. Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakati wa kufungua shampeni na baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa kwa kuwamiminia kwenye grasi zao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname