June 30, 2015 Dar es salaam: Katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani
na maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es salaam
maarufu kwa jina la Sabasaba, LG
Tanzania imetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei za bidhaa zake itakayodumu
katika kipindi chote cha ramadhani na Sabasaba.
Wateja
watakaonunua bidhaa za LG katika kipindi hiki cha ramadhani na Sabasaba watafurahia
punguzo la bei la hadi asilimia 15 pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo
zawadi za bure, alisema Meneja mwandamizi wa LG, Mr. Kim Taehoon.
Mr. Kim pia alitumia fursa hiyo pia kuitambulisha friji mpya ya LG yenye
milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish” kwa mara ya kwanza kabisa
katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises
Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini.
Alisema
friji hiyo ina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa kuzuia bakteria
na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama na wa kiafya, friji ina
makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, aina hii ya milango huja
pamoja na kioo imara. Friji hii inatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter
Compressor” ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Aliongeza
kuwa katika kipindi hiki cha maonyesho ya biashara ya Sabasaba, wateja wa LG
watajipatia ofa kabambe pale watakapotembelea banda la LG kiwanjani hapo ambapo
pia wataweza kupata bidhaa nyingine mbalimbali za LG ikiwemo friji jipya la
milango pacha aina ya “Velvet Gardenia and Coral Irish”
Bw. Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hiyo mpya iliyoingia
sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na uwezo wa friji hilo
huku akiongeza kuwa Friji hilo pia litapatikana katika maduka mengine yote yanayouza
vifaa vya kielektroniki jijini Dar.
“Katika kipindi hiki cha mfungo
mtukufu wa ramadhani, watu wengi hutunza vyakula vyao kwenye mafriji na ni
hulka ya wengi kuamka usiku kwa ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa
na manufaa sana kwao kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia
kutunza chakula katika hali ya usalama” alisema Kim.
Ofa hizi
zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na Sabasaba, hii ni
katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia bidhaa za LG zenye punguzo
la bei
“LG
Electronics daima inaendelea kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa
zenye ubora na muonekana yakinifu ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa
na toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa
zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya sokoni
ni muendelezo wa matoleo yetu ya teknolojia ambayo yanatengenezwa na kuboreshwa
kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja wetu” alisema Mr. kim Taehoon
LG Electronics, Inc
LG Electronics, Inc (KSE: 066570.KS) ni kampuni inayoogoza kimataifa kuleta teknolojia kwa matumizi ya umeme, mawasiliano ya simu na vifaa mbalimabli vya nyumbani. Tumeajiri takribani watu 87,000 kufanya kazi katika maeneo 113 duniani kote. Mnamo mwaka 2012 mauzo ya kimataifa yalifikia dola billioni 55.91 (KRW trillioni 59.04), LG inajumuisha vitengo vya biashara tano – vifaa vya burudani ya Nyumbani, Simu za Mawasiliano, Vifaa vya matumizi nyumbani, Viyoyozi vya majumbani & Nishati na kwenye Magari - na ni moja ya kampuni kiongozi wa kuzalisha TV Bapa, Vifaa vya simu, viyoyozi, mashine za kufulia nguo na friji. LG Electronics ni kampuni mwenzi wa 2013 ENERGY STAR ® .
Kwa habari zaidi kuhusu LG
Electronics, tafadhali tembelea
www.LGnewsroom.com.
LG Electronics, Inc (KSE: 066570.KS) ni kampuni inayoogoza kimataifa kuleta teknolojia kwa matumizi ya umeme, mawasiliano ya simu na vifaa mbalimabli vya nyumbani. Tumeajiri takribani watu 87,000 kufanya kazi katika maeneo 113 duniani kote. Mnamo mwaka 2012 mauzo ya kimataifa yalifikia dola billioni 55.91 (KRW trillioni 59.04), LG inajumuisha vitengo vya biashara tano – vifaa vya burudani ya Nyumbani, Simu za Mawasiliano, Vifaa vya matumizi nyumbani, Viyoyozi vya majumbani & Nishati na kwenye Magari - na ni moja ya kampuni kiongozi wa kuzalisha TV Bapa, Vifaa vya simu, viyoyozi, mashine za kufulia nguo na friji. LG Electronics ni kampuni mwenzi wa 2013 ENERGY STAR ® .
No comments:
Post a Comment