ULE msemo usemao ‘wagombanao ndiyo wapatanao’ umetimia kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kuwa na mgogoro kwa muda mrefu na baba yake, Abdul Jumaa ‘Baba D’ ambapo anadaiwa kusalimu amri na sasa wanaelewana, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukunyetishia.
Chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu wa Baba D, mapema wiki hii kililieleza gazeti hili kwamba, kwa sasa
Diamond amesalimu amri kwa baba yake kwani amekuwa akimsikiliza na kumsaidia pale anapokuwa na shida tofauti na ilivyokuwa awali.
Diamond amesalimu amri kwa baba yake kwani amekuwa akimsikiliza na kumsaidia pale anapokuwa na shida tofauti na ilivyokuwa awali.
“Angalau sasa Diamond anamsaidia baba yake kwani hata akimpigia simu anamsikiliza na anampa fedha ndogondogo za matumizi tofauti na zamani,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti kuu moja tu la kutochorwa jina gazetini
No comments:
Post a Comment