MSANII wa
filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina
la Farhad wanadaiwa kumwagana baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda
mrefu.Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Nisha na mpenzi wake
huyo ambaye walikuwa na mipango ya kuoana mwaka jana lakini ndoa
ikayeyuka waliachana kutokana na sababu zisizojulikana na sasa kila
mmoja yupo bize na maisha yake.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Nisha ili
kuzungumzia habari hizo ambapo alikiri kwamba ni kweli
wamemwagana.“Sababu za kuachana siwezi kuziweka wazi kwa sasa, niko
kikazi zaidi mambo ya mapenzi nimeyaweka pembeni nataka nitimize malengo
yangu ambayo hayakutimia mwaka jana,” alisema Nisha.
No comments:
Post a Comment