29 December 2013

HUU NDIYO UGONJWA UNAMTESA Jet Li, ANASEMA HATA HAWEZI KUFANYA MAZOEZI MEPESI

Muigizaji wa Martial art, Jet Li ameweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na ugonjwa unaosababishwa na kuzidi kwa madini ya chumvi mwilini (hyperthyroidism).

Je Li aliyetambulika rasmi kwenye ulimwengu wa filamu kwa filamu yake ya ‘Tai-Chi’, ameweka wazi hali yake ya kiafya hivi karibuni wakati wa kurekodi show ya Kichina ya kusaka vipaji  ambapo yeye ni jaji, kuwa anaugonjwa huo ambao ukizidi mtu huvimba sana shingo (Goiter).
“Nina hyperthyroidism, wakati mwingine ninaweza kupungua kilo 15 na wakati mwingine naongezeka tena kilo 15.”Alisema Jet Li.
“Nimenenepa sana sasa hivi. Huo ndio ukweli. Na sikuwa na nafasi ya kupungua kwa sababu dawa ninazotumia zinadhibiti uwezo wa moyo wangu, kwa hiyo siwezi kufanya mazoezi, ninasubiri hadi daktari atakaponiambia kuwa naweza kufanya mazoezi mepesi.” Ameongeza Jet Li.
Amekiri kuwa ugonjwa huo unamuumiza sana na kwamba yeye ni mtu wa kawaida tu na sio shujaa kama wanayemuona kwenye filamu akiigiza maisha ya mashujaa waliowahi kupita China kama Wong Fei Hung, Huo Yuan Jia.
“Mimi sio shujaa, mimi ni kama nyie tu, ninapata maumivu lakini sijadhoofika. Ninafuraha.” Amesema Jet Li.
Muigizaji huyo ni moja kati ya waigizaji walioiweka juu filamu iliyojaa mastaa ya ‘The Expendables’ inayoratibiwa na Sylvester Stallone aka Rambo. Na ataonekana pia kwenye Expendable 3 akiendelea kushikilia nafasi yake kama Yin Yang.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname