11 May 2015

ZARINAH HASSAN THE BOSS LADY NA MADAM RITA NI NDUGU

Kumbe! Machoni pa wengi maswali yaliibuka miongoni mwa mashabiki wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ baada ya kumuona akiwa ‘klozi’ na Bosi wa Bongo Stars Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ kwenye shoo ya Zari All White Party iliyofanyika juzikati kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Madam Rita akiwa katika pozi na Zari walipokua kwenye Zari All White Party.Katika ‘iventi’ hiyo, Madam Rita alikuwa beneti na Zari hivyo baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kudhani labda Madam alikuwa kama bodigadi’ wa Zari ili kusaidia linapokuja suala la kumwaga ung’eng’e a.k.a kutema yai lakiniIjumaa Wikienda limefanya kazi yake na kubaini kwamba wawili hao ni ndugu kabisa. 


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname