Dereva mmoja wa taxi nchini
Singapore amepongezwa na kusifiwa kwa uaminifu na moyo wa imani baada ya
kukabidhi kitita cha zaidi ya paundi 500, 000 sawa na mabilioni ya
shilingi kilichokuwa kimesahaulika kwenye gari yake.
Dereva huyo Sia Ka Tian (pichani)
mwenye umri wa miaka 70 na ambaye amekuwa akiendesha taxi katika mji wa
Singapore kwa zaidi ya miaka 30, alikuwa amewashusha wapenzi wawili watalii
kutoka Thailand waliokukwenda kujivinjari nchini humo, baadae aligundua
katika kiti cha gari kuna mfuko mweusi ambao sio wa kweke.
Anasema alipoufungua alikutana uso kwa
uso na fedha nyingi zaidi ya dila milioni moja za Singapore na papo
hapo akaamua kuzipeleka katika ofisi ya serikali inayohusika na vitu
vilivyopotea na kuzisajili zikisubiri atakayeulizia.
Katika mahojiano na gazeti moja dereva huyo alipoulizwa kwa nini hakuingia mitini
na fedha hizo, alijibu kuwa kwanza pesa sio muhimu kwangu, pili pesa hizo sio za kwangu , akahoji kwanini nizichukue?
Inasemekana kuwa wale wapenzi watalii
walitoa taarifa ya kupotelewa na mzigo wao katika kampuni inayomiliki
taxi anayoendesha mzee Sia.
Haikuchukua muda taratibu zilifanyika kisha wakakabidhiwa kitita chao bila kupungua hata sumni.
Taarifa zinasema dereva huyo
amezawadiwa na kampuni yake ya taxi hizo na atakabidhiwa tuzo ya heshima
kwa uaminifu wake. Hata hivyo haijajulikana kampuni hiyo itampa zawadi
gani.
No comments:
Post a Comment