Kwa mujibu wa mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz, tweet zenye
hasira zilizoandikwa na Davido jana hazimhusu muimbaji huyo wa ‘My
Number One.’
Mitandao mikubwa ya Nigeria ikiwemo Pulse na News24 imeandika kuwa
tweets hizo ambazo Davido anamzungumzia mtu asiye na shukrani kwake na
kwamba kiama chake kinakuja, zimemlenga Diamond.
Meneja wa Diamond, Salam aka ML Eight ameiambia Bongo5 kuwa hakuna ugomvi wowote uliopo kati ya mastaa hao na kwamba wako poa.
Uhusiano kati ya mastaa hao wawili uliingia dosari siku ya fainali ya
shindano la Big Brother Africa ambapo baada ya Idris kushinda Davido
alitweet ‘And They Cheat Again’ na Diamond ambaye usiku huo alishinda
tuzo ya TFA za Nigeria aliijibu kwa ujumbe wa kuibeza.
Kufuatia tweet hiyo ya Davido, watanzania wengi walimshambulia kwa matusi na kumtaka aombe radhi kitu ambacho aligoma kufanya.
Tangu hapo, kumekupowepo na speculations kuwa uhusiano kati ya wawili
hao umevunjika na ndio maana imekuwa rahisi kwa wengi kuhusi tweet hizo
za jana zimemlenga Diamond.
Credit Bongo 5
No comments:
Post a Comment