Licha ya kuwa Diamond Platnumz hakuongozana na mpenzi wake Zari The
Boss Lady kwenda Nigeria Jumatatu hii, lakini kuna uwezekano mkubwa
wawili hao wakawa pamoja kwenye hafla ya ugawaji tuzo za michezo za
Glo-CAF Awards itakayofanyika Alhamisi Jan 8 jijini Lagos, ambapo
Platnumz ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza.
Zari The Boss Lady amepost picha (hapo juu) asubuhi ya leo Jumatano
(Jan 7) akiwa kwenye ndege na kuandika “Another day, another flight.
Stay blessed”, inayoashiria kuna uwezekano mkubwa akawa anaenda kwa baby wake Nigeria.
Diamond naye jana alipost picha zake mwenyewe (hapo juu) akiwa
anaonekana mpweke na kuandika, “Kuna mtu alikuwa mnyooonge na mpweke
jana…” hii inamaanisha mtu muhimu ambaye ni baby wake ndiye
anayekosekana.
Baada ya kuwa pamoja Uganda kwenye party ya Zari mwishoni mwa mwaka
jana, Zari na Diamond walisafiri pamoja kwenda Burundi na Rwanda na ndio
sababu kuna kila dalili pia watakua pamoja Nigeria licha ya kuwa
hawakusafiri pamoja.
No comments:
Post a Comment