Kuna
ile tabia ya wizi wa mabegi ambao hutokea mtu akiwa safarini, zile za
mtu kufungua begi lisilo lake, zote hizo dawa yake ni hii teknolojia ya eGeeTouch.
Smart Luggage Lock inafanya kazi kwa kutumia App inayowekwa kwenye smartphone augadget, ili kufungua utakachokifanya ni kuswipe simu yako juu ya lock hiyo.
Kampuni
iliyotengeneza kifaa hicho imesema imeamua kutengeneza kifaa hicho
badala ya kufuli kwa kuwa kufuli inaonekana kama matumizi yake ni mtindo
wa kizamani kwa wasafiri na pia hii huongeza usalama zaidi.
Mtumiaji
anayetumia lock hiyo lazima akumbuke alivyoswipe na iwe siri yake pia
kama ilivyo kwa matumizi ya password, lock ina battery ambayo inakaa na
chaji mpaka miaka mitatu, pia unaweza kuichaji kwa kutumia waya wa USB.
Unadhani hii kwa Bongo inaweza kusaidia?Tazama picha zake hapa
No comments:
Post a Comment