Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Asha Baraka.
MKURUGENZI wa
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
wamewatolea uvivu mastaa wanaojihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya
(mateja) na kuwataka waache wenyewe.
Wakizungumza katika
mahojiano maalum na mwanahabari wetu kwa nyakati tofauti, Januari 5,
mwaka huu, wakurugenzi hao walikiri kuwa tatizo la mastaa wanaobwia unga
ni kubwa na halitapungua kama juhudi za makusudi hazitafanyika.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Kwa upande wake Ruge, alisema asilimia kubwa ya watu ambao wanatumia
madawa ya kulevya walianza kwa kuvuta bangi na baada ya kuizoea ndipo
wakaanza kuchanganya unga kwenye msokoto na baadaye kujikuta wanajidunga
madawa ya kulevya.
“Kuna wasanii wengi sana
wanaotumia unga ukiachilia mbali hao kina Ray C, Chid Benz, Diouf na
Aisha Madinda (marehemu) ambao waliwahi kuripotiwa, tunawajua ingawa
hawataki kujianika, wabadilike,” alisema Ruge.
Mwanamuziki Mashuhuri wa Twanga Pepeta, Msafiri Diof.
Asha yeye alisisitiza suala hilo kwa kutoa mifano hai. Alisema kabla
Aisha Madinda hajafariki, alifanya kila juhudi za kumnusuru na utumiaji
wa madawa lakini kuna watu walikuwa wakimpiga vita na kujikuta
wakimtorosha.
“Huwezi amini jinsi ninavyopigania vijana wangu kutoka kwenye wimbi hilo
maana nilishawahi kumchukua Banza na Msafiri Diouf enzi hizo Muhimbili
(Hospitali ya Taifa) walikuwa hata hawajaanzisha kitengo cha kuwapatia
dawa za kuondoa sumu hiyo.
No comments:
Post a Comment