09 January 2015

OKWI AIFUNGULIA KESI YANGA, AIDAI SH MILIONI 107



SIKU moja baada ya uongozi wa Simba kutangaza kuachana na kipa Juma Kaseja, sasa unalazimika kupambana na kesi mpya dhidi ya kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi.

Kupitia mwanasheria wake, Kampuni ya Agaba Muhairwe & Co Advocates ya Kampala, Uganda. Okwi amefungua kesi akitaka Yanga imlipe kitita cha jumla ya dola 62,000 (zaidi ya Sh milioni 107).

http://api.ning.com/files/A8I8pebmYzrQ**cBQlBQVq4TstEowDCxUdtC5rmZJstAj9a21l2nJ2I7CpS0XJyID4YypC37Ss93vgNH8eZnbSm86RMFlq3F/OKWI2.JPGMgawanyo wa madai hayo umegawanywa mara mbili, ukianza na dola 50,000 ambazo Okwi anaidai Yanga aliposajili ikiwa alilipwa nusu yake.

Pili, mshahara wake, dola 12,000 ambao pia hakulipwa na Yanga. Jumla inakuwa dola 52,000.

Tayari Agaba Muhairwe & Co Advocates wamewasilisha barua yenye kumbukumbu namba AM/129/ea kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji.

Barua hiyo ya Januari 7, kopi mbili, moja imewasilishwa kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na nyingine kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Mwanasheria huyo wa Okwi amesisitiza kwamba hawatafungua kesi yoyote kwa kuwa wanatoa hadi Februari 15 kuwa wameishalipwa fedha hizo.

Sehemu ya barua hiyo inaonyesha barua ya juzi inakumbushia barua nyingine kama hiyo ambayo kampuni hiyo ya mwanasheria iliitoa na kutaka Okwi awe amelipwa hadi Desemba 15, mwaka jana lakini haikufanyika.

Maana yake, iwapo Yanga watashindwa kufanya hivyo watakuwa tayari kufungua kesi ya madai kuhakikisha wanapata fedha zao na haina ubishi watakwenda Fifa ambayo wameisha itaarifu kuhusiana na deni hilo.

Okwi aliondoka Yanga baada ya uongozi kumtema katika hatua za mwisho za usajili wa dirisha dogo na Simba ikamsajili, hali iliyozua tafrani kubwa. Baadaye TFF ilimpitisha Okwi kuichezea Simba na Yanga haikuwa imekubaliana na uamuzi huo.


Kopunovic: Waleteni hao Yanga

Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
BAADA ya kikosi cha Simba kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kishindo, kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Serbia, Goran Kopunovic, ametamka wazi: “Waleteni hao Yanga.”

Jumatano iliyopita, kocha huyo aliyejiunga na Simba hivi karibuni akichukua mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, alikuwa ni mwenye furaha kubwa baada ya kuishuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Taifa Jang’ombe.

Matokeo hayo yamempa jeuri ya kutamka hivyo kwa kusema kuwa yupo tayari kupambana na timu yoyote ikiwemo Yanga ambayo imeonekana kufanya vizuri pia.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kopunovic alisema kuishuhudia timu yake ilipocheza na Mtibwa Sugar yeye akiwa jukwaani, aligundua mambo mengi ya kiufundi yaliyokuwa na upungufu.

“Vijana wanajitahidi sana kuzingatia maagizo yangu, jambo ambalo linanipa matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano haya.

“Kuna mabadiliko makubwa tofauti na nilivyowakuta, hivi sasa wanaweza kupambana na timu yoyote ile kwenye mashindano haya na kuibuka na ushindi, hata hiyo Yanga wataifunga kama tukikutana nayo,” alisema Kopunovic

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname