Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika la ndege la taifa la
Falme za kairabu United Arab Emirates limetajwa kuwa na ndege salama
kuliko zote duniani .
Kwa mujibu wa mtandao maalum unaotoa tathmini ya usafiri wa anga wawww.AirlineRatings.com umeichagua
ndege hii kuwa moja ya ndege salama kuliko zote ulimwenguni kwa mwaka
2015 kati ya ndege 449 ambazo zimefanyiwa tathmini duniani kote ambapo
jumla ya ndege 149 kati ya hizo zimepewa hadhi ya nyota 7 kama ndege
bora katika huduma na usalama.
Mfumo wa kutathmini usafiri wa anga unazingatia vigezo kadhaa ambavyo
hutolewa kwa mamlaka rasmi za usafiri wa anga pamoja na taarifa za
mashirika ya ndege
Rais wa Etihad Airways ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo
James Hogan amesema kuwa siku zote shirika lake limekuwa mstari wa
mbele kuhakikisha kuwa usalama na huduma bora vipanewa kipaumbele na
watahakikisha kuwa wanaendelea kubaki kwenye nafasi waliyopewa na
mtandao huo wa thathmini za usafiri wa anga.
Kampuni ya Etihad Airways ina kituo chake huko Abu Dhabi ambako kuna
chuo cha mafunzo ya urubani na nafasi zingine kwenye tasnia ya usafiri
wa anga pamoja na wakandarasi wa ndege na pia sehemu hiyo ina karakana
kubwa ambako ndege za Etihad hutengenezwa
Mhariri wa mtandao ambao umetoa tathmini Geoffrey Thomas ameisifu Etihad
Airlines akisema kuwa kampuni hii ni mojawpao kwenye kundi dogo la
makampuni ya usafiri wa anga ambayo yana ubora kuanzia kwenye huduma
mpaka kwenye bidhaa .
No comments:
Post a Comment