Show ya Mkasi ya wiki iliyopita imetufanya tufahamu mambo 10 muhimu tusiyoyajua kutoka kwa Diamond kama ifuatavyo:
1. Yupo kwenye mazungumzo na label moja kubwa duniani ambao walimtafuta baada ya kufanya show ya Big Brother Africa.
2.Ana simu nne na moja ina line mbili, hivyo ana line tano.Simu yake huiweka silent muda wote kwakuwa zinapigwa muda mwingi. Anayo moja maalum ambayo watu wengi hawaijui.
3. Ana nyimbo 133 ambazo ameshazirekodi tayari.
4.Mama
yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku
mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza
mwanae.
5.Zamani alikuwa anapenda kurap lakini aliona ukirap huwezi kupata mademu.
Alipokuwa akiimba watu wengi walikuwa wanamkataza kwakuwa waliona hawezi.
6. Q Chilla ndiye msanii anayempenda zaidi na muda mwingi husikiliza nyimbo zake.
7. Anamaliza mjengo wake uliopo Tegeta Dar es Salaam.
8.Anapenda kuja kuwa kama Usher Raymond.
9.Anapenda
jinsi Dully anawasupport wasanii wachanga kwa kuwashauri na kuwapa moyo
kuliko wasanii wengine wakongwe ndo maana anasema huwa hachuji.
No comments:
Post a Comment