24 October 2014

Tunda Man afanyiwa mbaya Afrika Kusini, nusura akimbizwe hospitali. Soma mkasa mzima hapa.

TUNDA man
Show ya Tunda Man nchini Africa kusini jumamosi iliyopita iliharibiwa baada ya mtu mmoja kupuliza pepper spray ama pili pili iliyo katika mfumo wa kupuliza kwenye chupa za Perfume,
kwa mujibu wa Tunda Man anadai wakati tukio hilo linatokea yeye alikua anatumbuiza ndani ya Club moja Capetown ghafla yeye na mashabiki wakaanza kujiskia vibaya wengine walikua wanaanguka kwa kuishiwa pumzi na wengine wakaanza kukanyagana ili kuwahi kutoka nje hali iliyosababisha majeraha kwa wengine
ndipo ikabidi mabaunsa wa club hiyo waanze kuwasaidia waathirika akiwemo Tunda Man ambaye nae alishaanza kuwa katika hali mbaya, baada ya hali kutulia ikagundulika kuwa kuna mtu Raia wa Burundi alikua amepuliza Pepper Spray ndani ya Club, raia wakataka Tunda aendelee na Show lakini polisi wengi waliofika eneo la tukio walizuia show hiyo isiendelee, na aliyesababisha majanga hayo alikamatwa baadae akaachiwa kwa dhamana….

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname