24 October 2014

T.I AFUNGUKA MENGI KUHUSU TANZANIA CHEKI VIDEO HAPA

Clifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya nguvu katika jukwaa la Serengeti Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 mwakahuu katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyojionea Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya jijini New York na kituo cha redio cha Power 105.1kwenye kipindi cha Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000. 

T.I amelinganisha idadi hiyo ya kutisha kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho sio rahisi kutokea. 

Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa kwa T.I, ambaye amesema hakuwa anahofu chochote alipokuja Tanzania, zaidi zaidi alikuwa akifikiria kuhusu mpenzi wake.

“Afrika ni Kubwa ukilinganisha Nigeria ambayo kiukubwa ni kama Texas, idadi ya watu waliopo Nigeria inalingana nawatu waliopo Marekani. Sasa pata picha watu wote tuliopo Marekani tukusanyike Texas. Kama kuna waathirika wanne, idadi hiyo yote haiwezi kuathirika..”—T.I 

Video ya T.I akiwa katika mahojiano hayo nimeshare na wewe mtu wangu wa nguvu, unaweza kuitazama hapa.Kama kifaa chako hakisomi player hii>>>BONYEZA HAPA!

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname