22 October 2014

MTIFUANO..VITA NZITO HASWA: ALI KIBA VS DIAMOND

Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba akipafomu.

Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba huku waandaaji wa tamasha hilo, Clouds FM wakisigana na Times FM kumgombea msanii wa Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Risasi Mchanganyiko linakupa mchongo kamili. 
Kwenye shoo hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia. 
Chanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo na Davido wa Nigeria

“Ishu ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi, wakajipanga katika maeneo tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza vizuri azma yao ya kuharibu pindi Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai chanzo hicho. SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname