22 October 2014

DUNIA INA MAMBO: MUME AMSHTAKI MKEWE KWA WIZI WA MTOTO WAO. MKASA MZIMA UPO HAPA

Bw. Rashidi anayemshitaki mkewe, Fatuma Ally kwa wizi wa mwanaye Zainabu Rashidi. Kwa mujibu wa Rashidi anayeishi na familia yake maeneo ya Tandale-Yemen, Dar, sakata hilo lilijiri wiki mbili zilizopita baada ya yeye kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumchukulia mwanaye cheti cha kuzaliwa.

Jalada la kesi namba MAG/RB/8329/2014- WIZI kwenye Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar, limefunguliwa na mwanaume aitwaye Rashidi akimshitaki mkewe, Fatuma Ally akimtuhumu kwa wizi wa mwanaye Zainabu Rashidi aliyemwandikisha jina la mwanaume mwingine aliyetajwa kwa jina la Paulo Mlela. 

Rashidi alisema kwamba alipofika Muhimbili alishangaa alipojikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa kwa muda na madaktari akidaiwa ni mwizi wa mtoto.Alisema, aliwaonyesha kadi ya kliniki ya mtoto Zainabu yenye jina lake (Rashidi) akiwa ndiye baba mzazi wa mtoto huyo, jambo ambalo madaktari hao walilishangaa.SOMA ZAIDI HAPA>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname