
1.Sisi
tumechukulia sehemu ya mashindano,uzuri sisi tuliambiwa na uongozi wa
Clouds kabla ya Diamond hajapanda ilikua saa 3 kamili tukaitwa
tukaambiwa kuna watu wamejiandaa kumzomea Diamond.
2.Kama
uongozi tulikaa na msanii wetu na kumjenga kisaikolojia na kumwambia
kuna hivi vinatokea wao walitaka aanze Davido kisha afate Diamond
kupunguza watu watakaozomea tukasema hapana pangeni show yenu kama
ilivyokuwa ni sehemu ya mashabiki kufurahi.
3.Hatujaathirika
kwamba msanii wetu ameshuka tunapoona watu wanapiga kelele kwa ajili
yako au huna sifa ile unatakiwa uangalie umekosea wapi unaenda
wapi,hatuna makosa kwa mashabiki wetu.
4.Kikubwa
Diamond anafanya vizuri tunatakiwa kuhamisha macho yetu tumpigie kura
Diamond kwenye tuzo za Channel O Music Awards, kwa sababu mwisho wa
siku chema chajiuza kibaya chajitembeza
No comments:
Post a Comment