24 October 2014

DIAMOND ASALIMISHA MAGWANDA POLISI

DIAMOND ASALIMISHA MAGWANDA POLISIMSANII wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond', amekiri kuhojiwa na polisi baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa mavazi yanayoaminika kuwa ni sare (magwanda) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hata msanii huyo alidai kwamba mavazi hayo hayakuwa sare za jeshi hilo na kwamba yeye aliyanunua alipokuwa Ujerumani ingawa baada ya kuhojiwa aliyasalimisha.

Diamond alipanda jukwaani Jumamosi iliyopita katika onyesho la Fiesta jijini Dar es Salaam akiwa na mavazi hayo jambo ambalo liliibua mjadala.
Akizungumza jana Alhamisi, Diamond alikiri kupata ujumbe uliomtaka kufika Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na madansa wake akiwa na nguo hizo.
"Awali Meneja wangu alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na madansa wangu ambao pia walizivaa, nilifanya hivyo na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname