24 July 2014

Kilichoendelea kesi ya Mbasha Mahakamani

KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo
mkewe Flora hakuwepo nyumbani.Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.Soma zaidi>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname