KATIKA
kuelekea sikuu za Krismasi na Mwaka mpya pilika pilika zimeongezeka
katika mji wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla huku vibaka pia
wakiendelea na udokozi na wizi wa vitu mbalimbali.
Katika
kuthibitisha hilo juzi Tanzania Daima limeshuhudia mkazi wa kijiji cha
Nshara, Machame wilayani Hai,ambaye jina lake halikupatikana mara moja
amenusurika kuuawa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira
kumshambulia kwa silaha za jadi baada ya kuiba kitoto cha nguruwe
maarufu kama "Kiti moto".
Tukio
hilo la aina yake ambalo linaashiria maandalizi ya siku kuu hizo
lilitokea juzi majira saa 5.30 asubuhi kijijini humo baada ya mkazi huyo
kuonekana akiwa amembeba mnyamya huyo begani akiwa katika mfuko,maarufu
kama Sandarusi mithili ya mzigo wa kawaida.
Akizungumzia
tukio hilo,mkazi wa kijiji cha Nshara, Husein Mbaruku alisema mtu huyo
alionekana akinyata katika banda la Nguruwe akiwa na mfuko wake akiamini
kuwa hakuna mtu aliyemuona ingawa wenyeji nao walikuwa wakimvizia ili
kuona anachotaka kufanya.
No comments:
Post a Comment