Baada ya kugoma na kuamua kutoka nje ya bunge la katiba Dodoma kikundi cha umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kimekutana na waandishi wa habari April 17 2014 na kuyazungumza haya yanayofata hapa chini.
Profesa Ibrahim Lipumba >>> ‘Tumekubaliana kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja Wabunge wote ambao hatuna dharura tutakua tumekwenda Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara kuanzia saa nne asubuhi, tutaondoka na boti asubuhi saa moja kuelekea Zanzibar na tutaeleza yaliyojiri katika bunge hili maalum’‘Baada ya hapo tutaendelea na mikutano nchi nzima kujulisha Wananchi msimamo wetu ambao ni rahisi, uko wazi kwamba Rais aliunda tume ya katiba katika utaratibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba itayokusanya maoni ya Wananchi lakini katika yale mapendekezo ambayo yamekuja ukawa ni mjadala wa matusi, kejeli, lugha za kibaguzi na kutaja Wapemba, Waarabu, Wakongo na Wahindi, viongozi wapo na hamna aliewakanya tena ndio wanawapigia makofi
Freeman Mbowe: ‘Tume iliundwa kuratibu zoezi kupata mawazo ya Wananchi kufanya utafiti ambao uliipa tume rejea maalum ya kufata, tume haikukusanya tu maoni ya Wananchi bali ilifanya pia tafiti nyingi na ilikua na timu kubwa tu ya watu makini na mahiri na ikaonekana muafaka wa muungano wa kudumu ni serikali tatu’
No comments:
Post a Comment