10 March 2014

Mwanaume avuliwa nguo na kuvishwa kanga na kisha kutembezwa mtaani baada ya kufumaniwa na mke wa mtu....


Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Salum Athuman (22), amejikuta akivishwa kanga na kutembezwa mitaani baada ya kwenda nyumbani kwa mwanaume mwenzake, Dastun Mkereti (26) kwa lengo la kujivinjari na mke wa mtu, Stela Ramadhan (20), akafumaniwa.
Tukio hilo lililofunga mitaa lilijiri maeneo ya Temeke, Dar, hivi karibuni na kugeuka sinema ya bure.
Ilidaiwa  kuwa jamaa huyo amekuwa akimsumbua mkewe kwenye simu kwa kutaka waonane ili wavunje amri ya sita huku akijua fika kuwa Stela ni mke wa mtu na alishapewa onyo mara nyingi na mwenye mke.
Ilielezwa  pia  kuwa cha kushangaza, pamoja na mwanamke huyo kubadili namba ya simu, wiki iliyopita jamaa alimpigia Stela kisha akamsisitiza waonane, ikibidi alale naye siku nzima kwa kuwa alikuwa anataka kukumbushia enzi zao kwa sababu aliwahi kutoka naye kimapenzi, kipindi cha nyuma kabla hajaingia kwenye ndoa.
 
Mkereti alisema kwamba baada ya kuona ndoa yake iko shakani kutokana na pepo la usaliti kumnyemelea mkewe, alimwambia mama watoto wake amruhusu kidume huyo waonane, ikibidi wakutane nyumbani kwake kwa kumdanganya kuwa haishi naye kwa sasa japo ndoa yao bado changa.INAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname