21 February 2014

HAYA NDO MANENO YA MATUSI KWENYE NGUO YA DIAMOND ...YALIYO SABABISHA VIDEO YA DULLY KUFUNGIWA

 
Wote tumemsikia jana Prince Dully Sykes akiongelea kufungiwa kwa video yake ya kabinti special na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) . Kuna sababu kuu mbili zilizosababisha video hii kufungiwa na ya kwanza  ni kitendo cha msanii Diamond Platnumz kuvaa T-shirt iliyoandikwa neno ambalo ni tusi  . Hii ingekua kwa nchi za mbele basi ungekutwa t-shirt hii wanaifanyia kitu kinaitwa “blurring” yaani
wanayafanya maneno yasisomeke lakini wabongo wakaona isiwe tabu na director akaamua kuacha video irushwe ikiwa katika hali hii.Sababu ya  pili ni vazi la ufukwe yule demu alilovaa kitu ambacho dully ameona haikua mbaya.
Je, Unadhani ni haki video hii kufungiwa na kama ni haki je unafikiri  ifungiwe ni kwasababu ipi ya msingi?

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname