29 December 2013

DUDE "NIMECHEZEA MAKOFI YA KUTOSHA SANA KWA MPENZI WANGU PINDI ASIKIAPO TETESI NATOKA NA DEMU MWINGINE"


MSANII wa filamu Kulwa Kikumbi aalitoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa alikuwa anapigwa na mkewe pale aliposikia tetesi kuwa katoka na demu mwingine. Dude alibainisha hayo pale alipoulizwa na Swahilitz swali la kizushi kuhusu kuishi na mzazi mwenzie Eva kwa kipindi kirefu bila ndoa "Siwezi kumwacha Eva bila ya kufunga nae ndoa, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa napigwa na Eva nami namwachia tu kwasababu nilikuwa najua kuwa ananipenda na ndiyo ,aana ananililia wivumimi tu", alisema Dude
Aliongeza kwa kusema kuwa anavumishiwa mambo mengi sana kuhusu Eva lakini wanayamaliza kwakuwa wanapendana na amemzalia watoto.
"Unajua mtu anapokaa na kutaka kinichafua kwa mke wangu ujue anajisumbua katika maisha yake na kwa taarifa ni kwamba natarajia kuao mwezi wa nne mwakani ili kufunga midomo ya wambea" alimaliza kwa kusema Dude

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname