29 December 2013
KUMBE CHANZO CHA DIAMOND NA PENNY KUACHANA SIO WEMA...NI KIGOGO MMOJA WA CCM NDIYE ANAHUSIKA
Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya Naseeb Abdull 'Diamond' na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Penny! Swahilitz inakupa full details
Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba fedha anazo.
Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo huyo kula vya watu
"Amini kwamba katika kipindi chote cha mahusiano yao, Diamond hajawahi kusalimiana na mama yake Penny hata siku moja, hata kaka zake Penny hawataki kabisa kumsikia Diamond na mara kibao wamekuwa wakimsema sana Penny kuhusu Diamond" kimesema chanzo chetu
Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya kuishi na Diamond
"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye aliyemshinikiza kwenda kuzika"
"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?
"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho
Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa akiishi na Wema.
"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.
"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"
Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!" kilisema chanzo hicho
"Kimsingi huyo kigogo niliyewatajia ndiye anahudumia Penny , fanyeni utafiti mtagundua" kilimaliza chanzo hicho
Baada ya kupata taarifa hizo Swahilitz ilimpigia Simu Penny ili kuweka sawa taarifa hizi lakini iliita bila kupokelewa.
Jitihada za kumhoji kigogo huyo zinaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment