29 December 2013

HUYU NDIYO MSANII ANAE TUHUMIWA KUTOKA KIMAPENZI NA NDUGU ZAKE WA DAMU WAKATI MKEWE AKIWA YUPO MAREKANI..!!


Mitandao mbalimbali ya Naija ikiwa ni pamoja na nigeriafilms na gossipnigeria imeripoti tuhuma nzito juu ya muigizaji maarufu wa Nollywood, Desmond Elliot ambaye ni mume wa mtu na baba wa watoto mapacha.
Desmond anatuhumiwa kuwa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na ndugu wa damu moja ambao ni warembo na half caste, Roseline na Yvette Muere na kwamba ameonekana akijiachia na mmoja mmoja katika sehemu na nyakati tofauti.
Kwa mujibu wa mtandao wa nigeriafilms, marafiki wa karibu wa muigizaji huyo wamesema kuwa jamaa amekuwa akitoka nao kwa siri ili wasijue mchezo huo. Ambapo mara ya mwisho ameonekana akiwa na Roseline Muerer katika hotel moja inayoitwa Intercontinental ya Lagos, walipoenda kuhudhuria tukio linalohusu filamu za Nollywood.
Imeripotiwa kuwa waliingia ndani ya ukumbi kila mtu kivyake ili kuwachanganya watu wasijue kama walikuja wote.
Muigizaji huyo ambaye ana mke aliyemzalia watoto mapacha hivi karibuni, amekuwa akionekana na mdogo wake Roseline, yaani Yvette ambapo mara ya mwisho wameonekana wakienda kuangalia movie kwenye jumba la cinema lakini pia wameonekana wakizunguka pamoja kwenye gari la Desmond katika maeneo tofauti.
Chanzo kingine kimeliambia National Enquirer ya Naija kwamba kuna wakati mdogo mtu amekuwa akitoka kisiri kwenda matanuzi na Desmond bila kumtaarifu dada yake ambaye angalau uhusiano wake unaonekana kufahamika na baadhi ya watu akiwemo mama yao mzazi.
Ripoti hizo zinadai kuwa matanuzi haya yote yamefanyika kwa kasi wakati ambapo mke wa Desmond akiwa Marekani ambapo alienda kwa ajili ya kujifungua mapacha wake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname