07 November 2013

RAY AELEZA SABABU ZA WASANII WA BONGO KUIGIZA MUVI ZA MAPENZI....


STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua ya filamu husika kufungiwa.
“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu. Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam hawakunielewa mpaka baadaye. Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza filamu za mapenzi tu,” aliema Ray.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname