Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto
ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa
ktk orodha ya mwanzo kabisa.Ktk utafiti binafsi sifa hii imetajwa na
wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.Lakini kwa
wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa
sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2
Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke
Lakini kwa nini wanawake au mabinti
hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa? Je ni kweli ni
watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa
kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya
20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK
MAHUSIANO..."
Siku zote,mwanamke anapenda awe huru
kwenda apendapo au kupewa atakacho.Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume
mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.Akikutana na
mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha
mume/mpenzi kama rimoti control.
Jambo wanalosahau wanawake ni
kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona
kundi hili la kuchuna wapendavyo.
Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli,,ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.
No comments:
Post a Comment