NIMEBUSU BUSU WENGI BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND NA HASHEEM THABIT ILA FOR NIKO SINGLE GIRL "JOKATE"
So
baada ya kuona headline kwenye Jarida la VibeTz ambalo liko mitaani
kuanzia leo October 18 2013 kuhusu Jokate kuzungumzia kwa mara ya kwanza
uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji Diamond Platnumz na mcheza
kikapu Hasheem Thabeet, J amekubali pia kuzungumza na millardayo.com na
kuweka wazi baadhi tu ya vitu vichache kati ya vingi alivyoongea na
VibeTZ.
Yafuatayo ni maswali machache ya Millard Ayo kwa Jokate:
Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?
Jokate:
Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo,
hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua
kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.
Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
Jokate:
Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment
na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki
wangu kutokunielewa.
Millard Ayo: umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..
Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu
Millard Ayo: Na wa Diamond?
Jokate: Oooh kipindi kifupi
sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila
kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate
yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media
saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au
wanaviwasilisha sivyo.
Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
Jokate: Yeah,
kwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua lakini
nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo
nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa
fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi
nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume
wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa
sasa hivi.
Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?
Jokate: Yeah,
kwa zaidi ya mwaka mmoja… sijawa na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh
this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi….
hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata
mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale..
SOURCE: MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment