22 October 2013

MSANII WA BONGO MUVI IRENE PAUL KUOLEWA BILA MAHARI...!!


MKALI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amesema wakati wake wa kuolewa ukifika, hatatolewa mahari kama ilivyozoeleka badala yake atachukuliwa bila ya mume kugharamia.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Irene alisema linapokuja suala la kuolewa huwa haoni maana ya mahari kwani mahari inayotolewa haiwezi kufika hata theluthi ya malezi ambayo wazazi walimlea.

“Kama tumeafikiana kuoana na mchumba wangu sitahitaji mahari kabisa maana kwa upande mwingine naona kama ni kutugeuza kama watumwa sisi wanawake,” alisema Irene Paul.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname