Mapigano mapya yamezuka jana
Jumamosi(26.10.2013) kati ya majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
na waasi katika siku ya pili ya machafuko ambayo yamesababisha miito ya
utulivu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa .
Mapigano ya hivi karibuni mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamezuka siku ya Ijumaa, chini ya wiki
moja baada ya serikali mjini Kinshasa na waasi wa kundi la M23 kutangaza
kuwa mazungumzo ya amani mjini Kampala yamevunjika.
Jeshi la serikali jioni ya Jumamosi
lilisema kuwa limeukamata mji wa Kibumba , mji ulioko kilometa 25
kaskazini ya eneo mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Goma ambao unatoa
njia kuelekea katika eneo la waasi upande wa kaskazini.
"Kibumba uko chini ya udhibiti wa jeshi
la serikali FARDC kuanzia leo," afisa mwandamizi wa jeshi ameliambia
shirika la habari la AFP mjini Goma. Waasi hawakuweza kupatikana mara
moja kuzungumzia tamko hilo.
Upande mwingine wa mapigano umeanza
ghasia siku ya Jumamosi wakati jeshi liliposhambulia maeneo ya kundi la
M23 katika jimbo la Mabenga, kiasi ya kilometa 80 kaskazini mwa goma na
karibu na mpaka na Uganda.(P.T)
Jeshi "limeanzisha mashambulizi katika
barabara ya Mabenga kuelekea Kahunga. Linatumia wanajeshi, vifaru na
makombora", afisa mwingine wa jeshi amesema, akizungumza kwa masharti ya
kutotajwa jina.
Waasi wamethibitisha kuwa mapigano yamesambaa hadi katika eneo la kaskazini.
Mapigano yasambaa
"Mapigano yanaongezeka katika maeneo yote," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa amesema katika tovuti ya kundi hilo.
Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon katika mzozo huo, Mary Robinson na Martin Kobler,
wametoa taarifa wakielezea wasi wasi wao mkubwa kuhusiana na mapigano
hayo mapya.
"Tunatoa wito kwa pande zote kuonyesha
hali ya uvumilivu na kuanza tena majadiliano mjini Kampala," wamesema.
Marekani imesema kuwa imesitushwa na ripoti za kuongezeka kwa mapigano,
licha ya miito ya kimataifa kwa pande hizo kuonesha hali ya kuvumiliana.
"Tunawasi wasi mkubwa juu ya ripoti za
mapigano ya mpakani, " katika jimbo la Kivu ya kaskazini, msemaji wa
wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki amesema katika taarifa, akizitaka
pande zinazopigana, "kuacha vitendo vitakavyozidisha hali hiyo".
Taarifa ya Psaki imezitaka pande hizo
kurejea katika majadiliano, " ili kuondoa vikwazo vilivyobaki kuelekea
kutiwa saini kwa makubaliano ya mwisho, na ya msingi, ambayo yataleta
usitishaji wa kudumu wa mapigano na kuwawajibisha wake ambao wamefanya
uhalifu mkubwa".
Jumuiya ya kimataifa yaonya
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja
wa Ulaya Catherine Ashton pia ametoa wito, "kwa wahusika wote katika
eneo hilo kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali hiyo na kuufanya mzozo huo
wa kimataifa".
Athari zilizoripotiwa ndani ya mpaka wa
Rwanda kutokana na matukio ya hivi karibuni yanapaswa kufanyiwa
uchunguzi kwa pamoja," amesema Ashton.
Waasi wanadai kuwa jeshi la serikali
lilishambulia maeneo yao mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi la serikali
linasisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza, madai ambayo yanaungwa mkono
na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo,
MONUSCO.
Wakati huo huo jeshi la serikali ya Congo
limesema limepata mafanikio makubwa dhidi ya waasi wa M23 katika siku
ya pili ya mapigano makali jana Jumamosi na kuitaka nchi jirani ya
Rwanda kusaidia kuwanyang'anya silaha waasi.
No comments:
Post a Comment