Na Gadness Mallya
Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa amejikuta akiangua kicheko
‘hevi’ baada ya kusikia taarifa za mwanaye kurudiana na aliyekuwa
zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza na mwanahabari wetu
juzikati, Baba Diamond alisema alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye
kurudiana na Wema kwani ndiye mwanamke anayejielewa na ana nyota kali
tofauti na warembo wengine aliowahi kuwa nao.
“Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).
“Hana majivuno hata mimi nilisema
mwanzoni walipoachana kuwa Diamond alipoteza bahati lakini sasa naamini
atafika mbali zaidi kwani kama siyo kuachana kwao, Diamond angekuwa
mbali,” alisema.
Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia
na Wema kwani ndiye mwanamke sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani
atashindwa kufanya mambo ya maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya
hapo alipo kwa sasa.
Hivi karibuni Diamond alithibitisha
kurudiana na Wema wakiwa China lakini alipotua Bongo akaendelea na
uhusiano wake na Penny hivyo kuwaacha mashabiki wake njiapanda
Source:GPL
No comments:
Post a Comment